Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amewalaumu maafisa wa usalama wa serikali ya  Kaunti ya Mombasa kwa madai ya kuwanyanyasa wananchi nyakati za usiku, hasa msimu ambao umekamilika wa sherehe za mwaka mpya.

Awiti amewalaumu maafisa hao kwa kuwatia mbaroni wananchi wasiokuwa na hatia wakati wa sherehe hizo katika fuo za bahari, kwenye vilabu na maeneo mengine.

Aidha, amemtaka Gavana wa Kaunti ya Mombasa Ali Joho na kamishna Nelson Marwa kuweka wazi majukumu ya maafisa hao wa kaunti, na iwapo wana haki kikatiba kufanya oparesheni nyakati za usiku na kuwatia mbaroni raia wasiokuwa na makosa.

Awiti ameyasema haya siku ya Jumapili baada ya kupokea malalamishi kutoka kwa wananchi wa eneo bunge lake kuwa wanahangaishwa na maafisa hao.