Share news tips with us here at Hivisasa

Mandugu wanne walitiwa mbaroni katika eneo la Ukakani, kaunti ndogo ya Yatta, kwa madai ya kuzua vurugu katika klabu.

Akidhibitisha kisa hiki, naibu wa chifu wa Kambi ya Ndege Francis Mutua, alisema kuwa wanne hao walifika katika kilabu hicho na kuagiza vinywaji.

Mutua alisema kuwa inadaiwa ndugu hao walizua vurugu pale walipoagizwa kulipia vinywaji hivyo.

Inaripotiwa kuwa wanne hao walimpiga mwenye kilabu hicho na kumuumiza,  pamoja na kuharibu mali ya kilabu hicho kwa kuvunja chupa na viti.

Wahudumu wa klabu hicho walisema kuwa kisa hicho kiliwasababishia hasara kwa vile wateja wao wengine walilazimika kuondoka.

"Badala ya kulipia vinywaji waliovyokunywa, walizua vurugu na iliwabidi maafisa was polisi kuingilia kati na kuwatia mbaroni,” alisema Mutua.

Naibu chifu huyo alisema kuwa wanaume hao sasa wanazuiliwa katika Kituo cha polisi cha Matuu wakisubiria kufikishwa mahakamani.