Mhariri mkuu wa gazaeti la The Star tawi la Mombasa, Maureen Mudi amesimama kizimbani kujibu madai kuhusu taarifa waliochapisha mnamo Disemba 23, 2015 kuwa kulipatikana bombu ndani ya jengo la mahakama kuu ya Mombasa.
Maureen amekubali kuwa waliandika na kuchapisha taarifa hiyo mbele ya jaji Dora Chepkwonyi siku ya Jumanne.
Maureen aliambia mahakama kuwa walifanya uchunguzi kuhusu taarifa hiyo na pia ameongeza kuwa kamanda mkuu wa Polisi Pwani alihakikisha kuhusu taarifa hiyo na kusema kuwa bado uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo.
Hatua hii inajiri baada ya wakili Hamisi Mwadzogo kuwasilisha ombi la kutaka wakuu wa gazeti hilo kufika mahakamani ilikueleza wapi waliopata habari hizo ambazo amezitaja kuhujumu haki na uhuru wa wateja wake.
Gazeti hilo liliandika taarifa kuwa kulipatikana bomu ndani ya jengo la mahakama ya Mombasa mnamo Disemba 10 mwaka jana wakati kesi ya wasichana wanne wanaokabiliwa na madai ya ugaidi ilipokuwa ikiendelea.
Aidha, liliandika kuwa waliambiwa na afisa wa kupambana na ugaidi ATPU kuwa anashuku wafuasi wa Al-shabab walihusika katika uekeja wa bomu hiyo.
Wakati huo huo Jaji Dora Chepkwonyi amevisihi vyombo vya habari kuwa makini katika kuandika taarifa zinazofanyika mahakamani.