Baada ya kushikwa na kuzuiliwa kwa takribani saa 30, msemaji wa chama cha ODM Philip Etale hatimaye aliacheliwa na kuelekea eneo bunge la Malindi alikoshikwa na maafisa wa usalama kwa madai kuwa laikuwa anashiriki kwenye utoaji wa rushwa.
Etale alishikwa mapema siku ya Jumapili kwa madai kuwa alikuwa anashiriki kwenye visa ambavyo vinaenda kinyume na sheria na utaratibu a upigaji kura nchini, na madai mengine ya kutaka kuvuruga mfumo wa mtandao wa tume ya kusimamia kura nchini IEBC.
Hata hivyo, habari hizo zimekanwa na Etale pamoja na viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga, wakidai kuwa serikali inajaribu kutumia vyombo vya usalama kuwanyamazisha, hatua ambayo wanasema haiwezi kuwatisha na kutoa imani kuwa kiti cha Malindi kitanyakuliwa na CORD.
Kulingana na OCPD wa Malindi ambaye aliongea na waandishi wa habari siku ya Jumatatu jioni, alisema kuwa wote ambao walishikwa kwenye visa vya utoaji rushwa walikuwa wanafanyiwa upelelezi na kutoa habari dhidi ya madai ya kuhusika kwenye visa hivyo kinyume na sheria.
Siku ya Jumatatu mapema baada tu ya kuanza rasmi shughuli ya upigaji kura, maafisa wengi wa kutoka mirengo ya JAP na CORD walishtumiwa kwa kuhusika kwenye visa vya kununua wapiga kura ambapo mbunge wa juja Robinson Gitau alishikwa akiwa na zaidi ya shilingi elfu 200 ambazo ilidaiwa alikuwa na nia ya kununua wenyeji ili kupiga kura upande wa JAP madai ambayo alikanusha.