Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mkuu wa polisi katika kaunti ya Mombasa wilayani Changamwe Joseph Muthee ameahidi kukabiliana na visa vyovyote vya uhalifu katika eneo hilo haswa eneo la Bangladesh.

Muthee amesema kuwa usalama utaimarishwa zaidi katika eneo hilo huku akiwaomba raia kushirikiana na mafisa wa polisi ili kuweza kukabiliana na wahalifu ambao wanazidi kuwa changamoto kwa wakaazi wa eneo hilo.

Mkuu huyo amenyosha kidole cha lawama kwa wakaazi, kwasabau wanaogopa kuwataja wahalifu ambao wamekuwa wakiawangaisha kwa mda mrefu huku akiwataka kuripoti ili kuwasaidia maafisa wake kuwatambua wahalifu hao.

Kitongoji duni cha Bangladesh kimekuwa kikikumbwa na visa vya utovu wa usalama majira ya usiku baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba pamoja na biashara za watu huku wakiwaibia mali yenye dhamani.