Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama kuu ya Mombasa imemuachilia huru mshukiwa wa mauwaji Mshenga Myumba, baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutekeleza mauwaji ya Amina Kenga Nyamawi, katika eneo la Kaloleni, mnamo Februari 2, 2014.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumanne, Jaji Martin Muya, alisema kuwa ushahidi uliotolewa unakinzana na kudhihirisha kuwa Mshenga hakuhusika katika mauwaji hayo.

Mshenga alikuwa amezuiliwa rumande tangu kushikwa kwake.

Mshtakiwa huyo alijawa na furaha na kutabasamu punde tu aliposikia kuachiliwa huru kwake.