Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Masaba kaunti ya Kisii, Elijah Moindi amewashauri wakaazi wa kaunti ya Kisii kutowachagua viongozi wafisadi na wasio na maendeleo katika uchaguzi ujao wa mwaka.
Himizo hilo limetolewa baada ya kubainika kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao hujihusisha kwa ufisadi na kusahau kufanya maendeleo jinsi inavyohitajika kwa viongozi.
Akizungumza siku ya Jumatatu katika eneo bunge Lakela, Nyaribari Masaba. Moindi alisema viongozi ambao wanastahili kuchaguliwa ni wale wanaoleta maendeleo wala si kujihusisha kwa ufisadi.
“Tunahitaji uongozi wa kuleta faida kwetu, naomba mnapopiga kura mwaka ujao mchague viongozi wa maendeleo na si wafisadi,” alisema Moindi.
“Naomba kila mkazi ambaye amefikisha miaka 18 awe na kitambulisho pamoja na kadi ya kura ili kujitayarisha kuchagua viongozi wenye maendeleo na kuondoa wafisadi uongozini,” aliongeza Moindi.
Mwanasheria huyo pia alikosoa wanasiasa ambao wanalahumu wakaazi kwa kujiandikisha katika maeneo bunge tofauti tofauti kando na pale wanapokaa huku akisema kila mtu ana haki ya kujisajili kama mpiga kura popote nchini.