Mwanafunzi mmoja kutoka shule ya wavulana ya Nyambaria kaunti ya Nyamira aliyejizolea alama ya A yenye pointi 84 amekiri kujiunga na kikosi cha wanajeshi.
Mwanafunzi huyo kwa jina Nelson Mogesa kutoka kijiji cha Nyamware alisema anahitaji kujiunga na kikosi cha wanajeshi ili kuokoa maisha ya wanainchi ambao hushambuliwa na kudhulumiwa na vikundi vya magaidi.
Akizungumza siku ya Jumapili mjini Nyamira, Mogesa alisema ndoto yake tangu alipojiunga na kidato cha kwanza imekuwa kujiunga na uanajeshi ili kuitetea nchi.
“Najihisi kuwa katika hali mbaya wakati nasikia watu ambao hawana makosa wanauawa kupitia magaidi," alisema Mogesa.
"Naomba kujiunga na kikosi cha wanajeshi ili kupambana na magaidi vilivyo na kupigania wale ambao hawana makosa,” aliongeza Mogesa.
Aidha, babake mwanafunzi huyo, Joseph Mogesa aliunga mkono ari ya mwanawe kwani haipo ndani ya uwezo wake kumlazimu kufanya taaluma asiyoipenda.