Polisi eneo la Tala wamemtia mbaroni mwanamume mmoja anayekisiwa kuendesha biashara ya pombe haramu katika eneo la Katine, kaunti ndogo ya Matungulu.
Akidhibitisha kisa hicho siku ya Ijumaa OCPD wa Matungulu Joseph Chesire alielezea kuwa maafisa wa polisi walipata habari kutoka kwa mkazi mmoja, na walipofika nyumbani kwa mshukiwa, walimpata na lita 80 za pombe haramu, na kumtia mbaroni.
Afisa huyo alisema biashara hiyo imekithiri katika eneo hilo la Tala ikilinganishwa na maeneo mengine katika kaunti ndogo ya Matungulu na maafisa wa polisi wamekuwa wakipata wakati mgumu kumaliza biashara hiyo.
"Maafisa wa polisi wamelazimika kuendeleza msako dhidi ya pombe haramu ili kujaribu kudhibiti biashara hiyo katika eneo hili,” alisema Chesire.
Chesire alimpongeza chifu was Tala Pius Nzioka kwa kuwa katikamstari mbele katika vita dhidi ya pombe haramu.
Vilevile aliwaomba wakazi kutoa habari kwa polisi kuhusu watu wanaojihusisha na biashara hiyo ya pombe haramu.