Share news tips with us here at Hivisasa

Mwili wa mwanamme mmoja aliyeripotiwa kupotea wiki moja iliyopita umepatikana ukiwa umeninginia mtini katika eneo la Kianjoya katika mpaka wa Gilgil na Njoro viungani mwa mji wa Nakuru.

Mwili huo ulipatikana na wapita njia Jumanne majira ya  asubuhi.

Joseph Kariuki Kiona aliripotiwa kupotea baada ya kufunga kazi yake majaira ya jioni wakati alipokuwa akielekea nyumbani kutoka kituo cha kibiashara cha Kianjoya anapofanya biashara ya kinyozi.

Hata hivyo inashukiwa kuwa mwii wa mwendazake ulikuwa na majeraha ya kukatwa miguuni na kichwani na huenda aliuawa Jumatatu jioni na kisha mwili wake kutupwa katika kichaka ulikopatikana.

Maafisa wa polisi wa kituo cha Mau Narok wameuchukua mwili huo na kuupeleka katika hifadhi ya hospitali ya jimbo la Nakuru.

Sarah koki ambabye ni OCPD wa gilgil amethibitisha kisa cha kupotea kwa mwendazake na kusema kuwa uchunguzi ulikuwa tayari umeanzishwa ili kubaini waliotekeleza mauaji hayo.