Mwanaharakati wa kisiasa Abdul Noor amewapongeza vijana mjini Nakuru kwa kujisajili kwa wingi katika shughuli inayoendelea ya usajili.
Noor alisema kuwa vijana katika kaunti ya Nakuru wamevunja rekodi kwa kujisajili kwa wingi kuliko wakati mwingine wote. Akiongea jumanne mjini Nakuru Noor amesema kuwa vijana wanaongoza katika idadi ya watu waliojisajili kufikia sasa.
"Vijana wamejitokeza kwa wingi sana na inafurahisha sana.
Wengi wa wale walijitokeza ni vijana na nawataka wazidi kufanya hivo na walete wenzao kujiandikisha,"akasema. Aidha Noor aliwataka vijana kutumia kura zao vyema wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
"Hata kama vijana wanajisajili kwa wingi ningewarai watumie hizo kura vyema kwa kuwachagua viongozi Swazuri,"alisema Noor.