Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amewakosoa vikali baadhi ya viongozi anaodai wamechochea wakazi wa kaunti ya Nyamira na Kisii kuzozana kuhusu mpaka wa kaunti hizo mbili.
Kulingana na gavana huyo, kuna baadhi ya viongozi ambao huchochea wakazi hao na wafanyibiashara kuzozana.
Akizungumza siku ya Jumatatu katika mji wa Nyamira, gavana Nyagarama aliwakosoa viongozi hao na kuwaomba kuacha siasa sizizo na maendeleo.
Nyagarama alisema walielewana na gavana wa kaunti ya Kisii kuwa soko la keroka litakuwa chini ya usimimizi wa kaunti hizo mbili.
“Soko la keroka linasimamiwa na kaunti mbili, hii yangu ya Nyamira na ile ya Kisii , wale viongozi wanaotafuta umaarufu kwa kuwachochea wafanyibiashara na wakazi kuzozana juu ya soko hilo la keroka ili kukosoa uongozi wa kaunti zetu si jambo la kufurahisha,” Nyagarama alisema.