Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wa Wadi ya Kiabonyoru, James Sabwengi, amewaomba maafisa wa polisi kuhakikisha kwamba usalama unadumishwa katika eneo hilo.

Haya yanajiri baada ya visa vya utovu wa usalama kuripotiwa katika eneo hilo.

Mwakilishi huyo vilevile amewaomba wakazi wa eneo hilo kushirikiana na maafisa wa polisi ili kuhakikisha kuwa visa vya ukosefu wa usalama katika eneo hilo vinadhibitiwa.

"Ningependa kuwasihi wakazi wa eneo hili kushirikiana na maafisa wa polisi ili kudumisha usalama kwa kuwa watu wanaotekeleza uhalifu wanaishi miongini mwenu,” alisema Sabwengi.

Sabwengi alisema kuwa tayari ameongea na kamishna wa Kaunti ya Nyamira Bi Josphine Onunga ambaye amemwahidi kushughulikia tatizo hilo.

"Tayari nimezungumza na kamishna wa kaunti Bi Josphine Onunga ambaye ameniahidi kulishughulikia swala hilo na pia nimeomba serikali kuu kununua gari litakalowawezesha maafisa wetu kupiga doria wakati wa usiku,” alisema Sabwengi.

Sabwengi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bajeti kwenye bunge la kaunti ya Nyamira alidai kuwa huenda polisi wanashirikiana na majambazi kuwahangaisha watu wa eneo wadi lake