Mwenyeki wa bodi simamizi ya zahanati ya kijamii ya Bondeni, katika Kaunti ya Nakuru ametoa wito kwa serikali ya kaunti kuhakikisha kituo hicho cha huduma za afya kimeboreshwa.
Akizungumza katika mahojiano siku ya Jumanne, Francis Shinali alisema kuwa kituo hicho kina umuhimu katika jamii na kinafaa kuimarishwa.
Shinala alisema kuwa serikali ya kaunti inapaswa kuajiri wahudumu wa afya wa kutosha na vile vile kununua dawa za kutosha.
Wakati huo huo, Shinali amewataka magavana kuzidi kushirikiana na serikali kuu kuhakikisha huduma za afya zinaimarishwa kwa manufaa ya wananchi.
Matamshi ya Shinali yanajiri siku chache tu baada ya baraza la magavana kutishia kuondoa baadhi ya huduma kutokana serikali kuu kukosa kuwasilisha fedha.