Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulikuwa na hali ya taharuki katika eneo la kwa Rhonda, Nakuru baada ya bomba linalosafirisha mafuta kutoka kwa kampuni ya Kenya Pipeline kupasuka na kupelekea kufuja kwa mafuta.

Inaarifiwa kuwa paipu hilo lilipasuka baada ya jamaa mmoja aliyekuwa akitengeza barabara moja (grader) iliyo katika mtaa huo wa kwa Rhonda kuharibu paipu hiyo. 

Peter Ondieki, mmoja wa wakaazi wa eneo hilo aliyeshuhudia kisa hicho aliwaambia wanahabari kwamba alikuwa miogoni mwa waliowaarifu maafisa wa polisi kuhusiana na tukio hilo.

"Niko na studio mahali ambapo mafuta yamemwagika. Wakati niliposikia mafuta yamemwagika, nilimpigia chifu na pia nikampigia simu mbunge Samwel Arama wa Nakuru Magharibi na kisha baadaye nikaona maafisa wa polisi wamefika katika eneo hili. Baada ya askari kufika, niliona maafisa wa shirika la msalaba mwekundu wamefika hapo na pia polisi pamoja na gari la kuzima moto," alisema Ondieki.

Tukio hilo la hii la ijumaa saa sita lilipelekea baadhi ya watu kujaribu kufika katika eneo hilo lakini maafisa wa polisi waliingilia kati na kuwazuia kabla ya gari la zima moto kutoka kwa kampuni hiyo na lile la kaunti ya Nakuru kufika katika eneo hilo.

Mkuu wa polisi wa Nakuru Musa Kongoli aliyeongoza zoezi hilo kwenye taarifa kwa wanahabari alikariri kwamba uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na kisa hicho.

Aidha, amekariri kwamba hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo huku akihimiza uma kutokimbilia maeneo ambayo matukio sawia huenda yakatokea ili kuzuia maafa ambayo huenda yakatokea.

"Tunafuraha kwamba wakaazi wa Rhonda walitujulisha kwa wakati kuhusu tukio hili na tukafika kwa haraka kudhibiti hali. Haijabainika ni nini kilichosababisha kupasuka kwa bomba hili lakini tutafanya uchunguzi ili kubaini kilichotokea. Baadhi ya watu walijaribu kufika kwenye eneo hili lakini maafisa wa polisi waliwazuia huku wakiwajuza kuwa ni kwa usalama wao," alisema Kongoli.

Mbunge Arama ambaye alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika kwenye eneo hilo amesema ujenzi wa barabara hiyo iliyokuwa ikitengezwa umegharamiwa na mradi wa kuboresha makaazi duni au Kenya Informal Settlement Improvement Programme –KISIP

Aidha, amesema maafisa wa polisi walifika kwa wakati na kuzuia uma dhidi ya kuteka mafuta hayo.

"Hii barabara inatengenezwa na watu wa golden colour kwa ushirikiano na kisip. wamefika hapa kutengeza barabara nah ii paiupu kwa bahati mbaya ikapasuka. Inasemekana hii paipu inayobeba mafuta aina ya super ikipitia Nairobi, Eldoret, Kisumu. Nataka kupongeza maafisa wa polisi kwa kufika haraka kwenye eneo hili pamoja na maafisa wa Kenya Pipeline kwa kudhibiti hali," alisema Arama.