Share news tips with us here at Hivisasa

Vijana katika kaunti ya Kisii wameshauriwa kutotegemea pesa za wanasiasa ila kutafuta mbinu ya kupata pesa na kujiendeleza kimaisha .

Ushauri huo umetolewa baada ya kubainika kuwa idadi nyingi ya vijana katika kaunti ya Kisii hukaa barabarani na kupoteza wakati wao huku wakisubiri pesa kutoka kwa wanasiasa wanaopita.

Akizungumza siku ya Jumatatu mjini Kisii, mbunge wa Nyaribari Masaba Elijah Moindi aliomba vijana kutafuta njia ya kupata pesa kutoka kwa serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kufanyia biashara badala ya kutegemea pesa za wanasiasa.

“Idadi kubwa ya vijana hukaa barabararani kusubiri wanasiasa ili kuwapa pesa, hiyo ni njia moja ya kuunga mkono umaskini ambao huwezi kuisha miongoni mwetu,” alisema Moindi.

“Naomba kila mmoja wa kijana kujiunga kwa vikundi ili kupata pesa kutoka kwa serikali na kuanza kufanya biashara na kujiendeleza na kujiimarisha kimaisha , haya mengine ya kutegemea pesa za wanasiasa hayawezi kutoa usaidizi wowote,” Moindi aliongeza.