Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi wa vijana katika eneo la Lanet, eneo bunge la Bahati wametakiwa kutetea maslahi ya vijana badala ya kuangazia maslahi ya kibinafsi.

Katibu wa hazina ya CDF eneo bunge la Bahati ambaye pia ni mwakilishi wa hazina ya uwezo katika eneo la Lanet na viunga vyake Collins Oduor, alisema kila kiongozi wa vijana ana wajibu wa kuhakikisha kwamba maslahi ya vijana yanapewa kipaumbele kwa mujibu wa katiba.

Akizungumza katika eneo la Modern Lanet, Collins Oduor ametoa wito kwa vijana kutoka wadi mbalimbali za eneo bunge la Bahati kuhakikisha kwamba wanajitolea kutafuta maarifa kuhusiana na hazina mbalimbali walizotengewa na serikali.

Kwa mujibu wake, ukosefu wa maarifa kuhusiana na hazina hizo ndio unaowarejesha nyuma vijana katika maswala ya maendeleo.

“Taifa hili litasonga mbele iwapo vijana na akina mama watazidi kupokea usaidizi wa serikali kujikuza,” alisema.