Huku ujenzi wa kiwanda kipya cha majani chai kikianza kujengwa katika eneo la Matunwa wadi ya Gesima.
Mwanasiasa wa eneo bunge la Kitutu Masaba Victor Ogeto ameomba wakaazi wa wadi hiyo wakabidhiwe nafasi za kwanza katika kupata ajirakiwandani humo.
Kulingana na mwanasiasa huyo aliyezungumza katika wadi hiyo ya Gesima, wakaazi wa wadi hiyo wanastahili kufaidika kutokana na mradi huo ili kujiendeleza.
“Naomba wakaazi wa wadi ya Gesima wapewe nafazi za kwanza kufanya kazi katika kiwanda hiki ambacho kimeanzishwa hapa ili nao waweze kupata riziki ya kila siku na kujikimu kimaisha," alisema Ogeto.
Kwa upande wa wakulima wa majani chai wakiongozwa na Christopher Bosire walilalamikia kutochukuliwa kwa majani chai yao kutoka kwa vituo vya ununuzi jambo ambalo walisema limewasababishia hasara.
Wakulima hao waliomba majani chai kuchukuliwa kutoka vituo vya ununuzi kwa wakati unaofaa ili kupunguza hasara ambayo wanapata wanapopima uzani wa majani chai yao.
“Kile tunaomba ni kupunguziwa hasara, majani chai yetu yanapokaa kwa zaidi ya siku mbili bila kuchukuliwa kutoka vituo vya ununuzi ni hasara kwetu tunaomba yachukuliwe kwa wakati unaofaa,” alisema Bosire.