Aliyekuwa waziri wa ugatuzi, Anne Waiguru, amekanusha madai kuwa alipanga njama ya ufujaji wa fedha za shirika la huduma za vijana kwa taifa NYS.
Waiguru ametaja madai yaliyotolewa na Josephine Kabura kama yasiyo ya kweli na ambayo yananuia kumchafualia sifa na kuimaliza azama yake kisiasa.
Waiguru anadai kuwa hamfahamu Kabura wala hawajawahi kutana naye kama anavyodai katika stakabadhi alizowalisha mahakamani.
"Sijawahi kutana na Josephine Kabura na hata simjui. Usemi wake wa kuwa nilishirikiana naye kuiba pesa za NYS ni ya uongo na ninajua ni njama ya watu waliotajwa kuhusika na wizi huo wanataka kuniangamiza kisiasa," alisema Waiguru.
Juamtatu, kwenye kiapo kupitia stakabadhi alizowasilisha mahakamani, mfanyibiasha huyo alidai kuwa Waiguru ndiye mhusika mkuu wa sakata hiyo ya ufisadi kwani alifahamu kikamilifu yaliyokuwa yakiendelea.
Kabura anadai kuwa Waiguru ndiye alimsadia kubuni kampuni zake ambazo zilitoa huduma kwa shirika la NYS, kufungua akaunti kadhaa za benki na baadaye kupokea mamalioni ya pesa kama malipo na kuongeza kuwa alihusika katika njama ya kuficha ukweli wa sakata hiyo ilipofichuliwa.
Kabura aidha ameongeza kuwa waziri huyo alitambulika kwa washusika wengine kwenye sakata hiyo ambao angeshirikiana nao kufuja fedha hizo wakiwemo dadake Waiguru, Loise Mbarire, mshauri wa NYS, Mutahi Ngunyi , afisa mkuu wa wizara ya ugatuzi, Hassan Noor, afisa mkuu wa NYS, Adan Harakhe, na kiongozi wa kitengo cha uchunguzi katika benki, Joseph Mugwanja.