Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa kaunti ya Likoni wamelalamikia kero la kunguni ambalo limekithiri kwa muda mrefu sasa, japo kuwa wametumia dawa karibu zote madukani za kuangamiza wadudu hao.

Wakiongea na mwanahabari huyu, wakaazi hao wa eneo la Mwachamago wamesema kuwa wamekabiliana na tatizo hilo tokea mwanzoni mwa mwaka huu bila mafanikio yoyote. 

Mmoja wa wakaazi hao, Bw Ismail Salim amelalamikia kutowajibika kwa serikali ya kaunti hiyo kwani hawajashughulikiwa licha ya kutoa malalamishi kwa sekta husika ya afya.

Kunguni hao ambao kwa sasa wameenea hata kwenye magari ya usafiri wanawakosesha wengi usingizi kwani hufyonza damu nyakati za usiku. 

Hata hivyo wakaazi hao wameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuwanyunyizia dawa ya kuwaangamiza kabisa wadudu hao walivyoahidi awali katikati ya mwaka huu.