Share news tips with us here at Hivisasa

Wakatoliki katika Kaunti ya Nakuru wamehimizwa kuzidi kujisajili kuhudhuria misa itakayoongozwa na Papa Francis mnamo Novemba 26, 2015.

Himizo hilo limetolewa na Padre Evanson Njogu wa Parokia ya St Joseph’s the Worker iliyo mjini Nakuru aliyesema kungali nafasi zilizosalia kwa wale ambao wanataka kujisajili kuhudhuria misa hiyo.

Akizungumza baada ya ibaada katika Kanisa la Cathedral Church of Christ the King mjini Nakuru siku ya Ijumaa, Njogu ambaye pia ni padri msimamizi wa Dekania ya Nakuru alisema jimbo katoliki la Nakuru lingali linajiandaa ili kuhudhuria misa hiyo.

Kwa upande wake, askofu wa jimbo katoliki la Nakuru aliwahimiza wakatoliki kujiandikisha kwa wingi.

Kulingana naye, wale ambao hawatajisajili pia wanaruhusiwa kuelekea jijini Nairobi katika ibaada hiyo takatifu ya misa itakayoongozwa na Papa Francis.

Askofu huyo alisema kwamba watu ambao watakuwa hawajisajili hawatakuwa katika sehemu iliyotengewa wale waliojisajili katika uwanja wa Chuo kikuu cha Nairobi.

Papa Francis ambaye ni kiongozi wa kanisa katoliki duniani anatarajiwa kuwasili jijini Nairobi tarehe Novemba 27, 2015 kwa ziara ya siku tatu itakayofikia kikomo tarehe Novemba 27.

Baada ya kuondoka Kenya, Papa Francis ataelekea nchini Uganda.