Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa kata ndogo ya Geteri, Wadi ya Gesusu, wamelalamikia kukwama na kutojumuishwa katika miradi ya maendeleo katika wadi hiyo.

Wakizungumza siku ya Alhamisi katika eneo la Nyamesocho, kwenye hafla ya mazishi ya mwendazake Mochere Nyamoko, wakazi hao walimkosoa Mwakilishi wa Wadi ya Gesusu, Sammy Keronche, kwa kutowajumuisha wajumbe wao katika kamati ya miradi ya maendeleo.

John Nyabicha, mkazi, alidai kuwa mwakilishi Keronche huwajumuisha watu wachache katika miradi ya maendeleo na kuwasahau wakazi.

Diwani wa zamani wa eneo hilo, Bwana Elius Isoe, alisema kuwa vijana hawawezi kuwajibika katika uongozi bila kuwepo mwelekeo wa wazee.

Alimwomba mwakilishi Keronche kuwajumuisha vijana kwa wazee katika kamati mbali mbali za maendeleo

“Uongozi mzuri wa kuleta maendeleo ni ule wa kuwaleta wakasi pamoja na kutoa mwelekeo wa maendeleo yao katika jamii. Viongozi wa kisasa lazima wabadili jinsi ya kufanya shughuli za jumla ili kubadili sura za maeneo yetu,” alisema Maranga.

Wakazi hao walisema wanataka miradi ilioanzishwa na Balozi Sam Ongeri kukamilishwa kwa ushirikiano wa wakazi, mwalikishi wadi Sammy Keronche na mbunge wa Nyaribari Masaba Elijah Moindi.