Wakaazi wa eneo la Burgei katika kaunti ndogo ya Rongai,wametishia kufanya maandamano kutokana na ukosefu wa maji safi ya kunywa.
Wakizungumza Jumanne wakaazi hao walisema kwamba, walikuwa wakitegemea bwawa lililoko eneo hilo lakini sasa limefeli na linapaswa kutengenezwa.
Mmoja Wa wakaazi hao Kennedy Kilwa alisema kuwa, shida hiyo ambayo imewakumba kwa muda wa miezi miwili sasa imewalazimu kutumia Maji ya mto Molo ambayo sio safi kwa kunywa.
"Tangia bwala hili kuharibika, halijawahi kukarabatiwa na shida ya maji inazidi kutukumba," alisema Kilwa.
Aliongeza kuwa, Maji ya bwawa hilo yalikuwa yakifaidi shule, wananchi na hata kituo cha afya cha Rongai.
Naye Milka Cherono amesema kuwa, wamejaribu kuwasilisha malalamishi haya kwa MCA wa Wadi ya Visoi lakini hadi sasa hawajapata usaidizi.
"Tumewasilisha malalamisha mara kadha lakini hakuna lolote limefanywa," alisema Cherono.
Wametaka gavana Wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua kuingilia kati ili wapate usaidizi wa haraka.
Aidha, MCA Wa wadi ya Visoi Edward Gitau amekieleza kituo hiki kuwa ameweka mikakati ili kuhakikisha Kuwa tatizo hilo limetatuliwa.