Share news tips with us here at Hivisasa

Aliyekuwa mbunge wa Changamwe Ramadhan Kajembe amevitaka vyombo vya habari kutokubali kutumiwa na wanasiasa wasio na maadili kutaka kugonganisha watu kwa misingi ya vyama.

Kajembe alisema kuwa wakati huu ambapo taifa linakaribia uchaguzi mkuu, wananchi wanafaa kuwa kitu kimoja bila kutenganishwa kwa misingi ya kisiasa wala kikabila.

Kauli yake inajiri baada ya gazeti moja nchini kuchapisha taarifa kuwa Kajembe alimtukana kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Kwenye kikao na wanahabari siku ya Jumanne, Kajembe alikanusha madai hayo na kusema kuwa hio ni katika ya njama za kumuharibia jina, na kulitaka gazeti hilo kuweka wazi ni wapi na lini alitoa matamshi kama hayo ya kumkejeli Raila.

Kulingana na taarifa hiyo ni kwamba Kajembe alimtaka Raila Odinga kuweka wazi wapi alipopeleka pesa alizopewa alipokuwa ng’ambo, baada ya Odinga kumtaka Naibu wa Rais William Ruto kufanyiwa ukaguzi wa maisha yake.