Mahakama ya Mombasa imewaachilia huru wanakamati watatu wa hazina ya CDF wa eneo bunge la Lamu Magharibi, baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha wa kuwahusisha na ukiukaji wa kanuni za ununuzi wa bidhaa.
Watatu hao, Mohamed Bute Galgalo, Bakari Mohamed Omari na Nassir Bwanamkuu Abdalla wanakabiliwa na shtaka la kukiuka kanuni za ununuzi mnamo Novemba 7 mwaka 2007.
Watatu hao wanadaiwa kuagiza kununuliwa kwa tingatinga saba za eneo bunge hilo, pasi kushirikisha kampuni nyinginezo katika kutoa maombi yao ya kandarasi.
Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, Hakimu mkuu wa Mahakama ya Mombasa Susan Shitub alisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha wa kuwahusisha watatu hao na mashtaka hayo.