Share news tips with us here at Hivisasa

Washukiwa wawili wa wizi wa mifugo walitiwa nguvuni Jumanne baada ya kupatikana na ng’ombe wawili waliokuwa wameibiwa katika eneo la Kajulu.

Wawili hao, Ramano Kiburimo na Amos Kipkosgei inadaiwa walipatikana na ng’ombe wawili wa wizi.

Taarifa iliyoandikishwa katika kituo cha polisi cha Kondele imearifu kuwa wizi wa ng’ombe hao ulitekelezwa mnamo Januari 16, 2016.

Akithibitisha kisa hicho OCS wa Kondele, Baraza Khan alisema washukiwa hao walikiri kutekeleza wizi huo.

''Ndio tumekamata wanaume wawili ambao wamekiri kuiba ng'ombe watatu na kwa sasa tumewazuilia katika kituo hiki cha Kondele na watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao,'' Baraza alisema.