Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama ya Mombasa imeagiza washukiwa wanne wa ugaidi kuzuiliwa korokoroni kwa siku 30, wakisubiri uchunguzi kukamilika.

Watuhumiwa hao, Mohamed Abdalla Kassim, Faraji Fahim Swalehe, Ali Omar Bwanadi na Kassim Ali walikamatwa mnamo Machi 1, 2016, katika eneo la Bumala Kaunti ya Busia, wakiwa safarini kuelekea Uganda na kuhusishwa na visa vya ugaidi

Siku ya Jumatatu, afisa wa upelelzi Samuel Ouma aliwasilisha ombi la kupewa muda zaidi wa kufanya uchunguzi wa madai hayo mbele ya hakimu katika mahakama ya Mombasa, Diana Mochache.

Ouma aliiambia mahakama kuwa anachunguza simu za washukiwa hao.

Wanne hao pia wanakabiliwa na kesi nyingine ya ugaidi katika mahakama ya Lamu.

Aidha, wanahusishwa na kisa cha kifo cha polisi na kupotea kwa bunduki katika eneo la Bondeni mnamo Oktoba 2, 2015.

Kesi yao itatajwa tarehe Aprili 7, 2016 baada ya kukamilika kwa uchunguzi.