Watu watatu walijeruhiwa Jumanne asubuhi saa kumi na mbili katika ajali ya barabani eneo la Egetai barabara kuu ya kisii-keroka. Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo waliseme kuwa gari hilo aina ya Nissan ambalo lilipoteza mwelekeo na kugonga kando ya barabara lilikuwa limebeba wanafunzi wanne pamoja na mwalimu mmoja ambao walikuwa wanaelekea katika chuo kikuu cha kisii.
“Tulisikia mlio kama wa bomu karibu saa kumi na mbili asubuhi tukakimbia kufika tukapata ni gari. Tulianza kutoa watu, wanafunzi wanne walikuwa wanaenda kisii campus na mwalimu mmoja. Kuna watatu ambao waliumia wakapelekwa hospitali ya Level 6," Paul Mogire alisema.
Waliopata majeraha wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya Kisii Level 6.