Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bweni ya wanafunzi wa Shule ya Upili ya Nyakongo Wilayani Masaba Kaskazini, Kaunti ya Nyamira ilishika moto mwendo wa saa 6 usiku wa kuamkia leo Jumatatu.

Akithibitisha kisa hicho siku ya Jumatatu asubuhi, mwenyekiti wa elimu katika Kaunti ya Nyamira Siroma Kinaiya amesema wanafunzi 71 walinusurika kifo kwa kutimua mbio wakati moto huo ulipoanza kushika bweni hiyo ghafla na kusema hamna aliyejeruhiwa.

Chanzo cha moto huo kwa sasa hakijabainika. Visa vya moto katika shule zilizoko katika Kaunti ya Nyamira vimeonekana kuongezeka kila wakati, jambo ambalo limewaacha wakazi wa kaunti hiyo vinywa wazi na kushindwa kulibaini hadi sasa.

Ni wiki moja tu imepita tangu Shule ya Upili ya Nyamaiya na Shule ya Wavulana ya Nyamira kushika moto na kuaribu mali ya thamani yasiojulikana.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa elimu katika Kaunti ya Nyamira Kinaiya uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo.

Kwa upande wa wakazi walioongea na Waandishi wa habari leo asubuhi, chanzo cha moto huo sharti kichunguzwe na kupashwa kwa wananchi kwani wamehofia ongezeko la moto kuteketeza baadhi ya shule katika eneo hilo wakiongeza kuwa huendea visa kama hivyo viongezeke.

“Naomba tuambiwe ni nini kinasababisha moto katika shule zetu maanake tumehofia kuwa watoto wetu watakufa kutokana na visa hivi,” alihoji Gladys Siro, mkazi wa Nyamira.