Vijana kutoka kaunti ya Nyamira wameiomba serikali ya kaunti hiyo kuwajumuisha katika ajira shughuli za maendeleo.
Wakizungumza siku ya Jumanne katika eneo la Nyambite Kaunti ya Nyamira, vijana hao, wakiongonzwa na James Kengoina walisema kuna idadi kubwa ya vijana katika kaunti hiyo waliohitimu katika taaluma mbalimbali lakini bado hawajapata ajira.
“Tunaiomba serikali ya kaunti hii ituhusishe sisi maana wengi wetu tuko na ujuzi lakini hatujawahi pata ajira katika kaunti hii yetu ya Nyamira,” alihoji Beatrice Onyiego.
“Mimi nimejaribu sana kutafuta ajira katika kaunti hii lakini sijafanikiwa. Kama wazaliwa wa hapa tunaomba serikali ya kaunti ituhusishe sisi vijana ana kutupa ajira,” alisema Gilbert Omuga.
Wakati huo huo, vijana hao waliomba vijana wengine kuungana pamoja na kuchukua mikopo ya serikali ya kaunti ili waweze kujiimarisha.
“Tunaomba vijana wengine wale hawakujumuika nasi leo waunganena kuchukua mikopo ya kuanzisha biashara. Tujitegemee, tuinue uchumi wetu,” aliongeza Omuga.