Bunge la Kaunti ya Nyamira limepokezwa ripoti ya kutowasimamisha kazi maafisa watatu na bunge hilo kwa madai ya ufisadi na utumizi mbaya wa ofisi.
Ripoti hiyo ilitolewa na mahakama ya viwanda baada ya maafisa hao kushtaki bunge hilo kwa kusema jinsi waliovyosimamishwa kazi sio halali.
Ripoti hiyo ilidhibitishwa siku ya Jumanne bungeni na Spika wa bunge la kaunti hiyo Joash Nyamoko pamoja na Karani wa bunge Daniel Orina.
Mishahara ya maafisa hao haitasimamishwa na nyadhifa zao hazitachukuliwa na mtu tofauti hadi kesi hiyo isikizwe na kuamuliwa.
kulingana na ripoti hiyo, maafisa hao wako na haki ya kuendelea kudumu afisini hadi kesi isikizwe na wasisumbuliwe vyovyote na bodi ya kuwaajiri wafanyikazi wa Kaunti ya Nyamira.
Maafisa waliohusishwa na ufisadi na utumizi mbaya wa ofisi ni Mkuu wa Idara ya Michezo na Utamaduni Peter Omwanza na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Fedha John Omanwa na Kefha Osoro.
Maafisa walioondolewa madai ya kujihusisha na sakata hiyo ya ufisadi kulingana na ripoti hiyo iliyosomwa na mwenyekiti wa jopo lilioundwa kwachunguza maafisa hao ni Mkuu wa Idara ya Barabara Kepha Osoro, Mkuu wa Idara ya Maji Andrew Ombati, na Fridah Nyaboga.