Share news tips with us here at Hivisasa

Mashindano ya mbio za shule za msingi kitengo cha Kitaifa yaling’oa nanga siku ya ijumaa katika uga wa chuo kikuu cha Kisii, kaunti ya Kisii.

Akiongea katika ufunguzi wa mashidano hayo katika uga wa chuo cha Kisii, mkuu wa elimu katika kaunti ya Kisii Richard Chepkawai aliwaomba washikadhau wote kushirikiana ili kuhakikisha kuwa mashidano hayo ya siku mbili yatakamilika kwa njia shwari.

Aidha, alizipongeza kaunti zote kwa kuhakikisha kuwa wanariadha waliofunzu kutoka kiwango cha maeneo wamefika katika mashindano hayo.

“Nawopongeza washikadhau wote kwa kufanikisha mashindano hayo, haswa kuwaleta wanafunzi hawa kutoka maeneo mengine hadi hapa Kisii,” alihoji Chepkawai.

Kwingineko, aliongezea kuwa ni imani yake kuwa watakaofunzu wataiwakilisha Kenya katika mashidano ya Dunia yatakayoandaliwa katika nchi ya Amerika.

Chepkawai aliwaomba wanariaadha wote waliofika kuwakilisha maeneo yao kufanya bidii ili kuhakikisha kuwa wamezonga mbele hadi kiwango kingine.

“Mwanariadha yoyote lazima atie bidii katika kazi yake, na lazima ajue kuwa akisonga kutoka kiwango kimoja hadi kingine kuna wapinzani wakubwa, kwa hivyo lazima ajitahidi ili kunawiri,” Chepkawai aliwaambia wanariadhaa.

Mashidano hayo yanafanyika katika uwanja wa Chuo cha Kisii katika kaunti ya Kisii kwa siku mbili, huku majiombo yote nane yakishiriki.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Kuandaa mashidano hayo katika kaunti ya Kisii Yophes Kegochi aliwakikishia wageni kuwa kuna usalama wa kutosha na wanastahili kujihisi wamo nyumbani.

“Nawakaribisha katika mashidano haya na mjihisi kuwa mko nyumbani ili tuweze kufanya shughuli hii kwa pamoja,” aliongezea Kegochi.