Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mara nyingi siku ya Jumatatu kama leo, mji wa Kisii hukumbwa na msongamano wa magari kutokana na umati wa watu wanaoenda katika soko la Daraja mbili aidha kuuza au kununua bidhaa.

Kutokana na msongamano huo, wakazi wa mji huo wameiomba serikali ya Kuanti ya Kisii kufungua baadhi ya barabara katika mji huu ili kurahisisha uchukuzi katika mji huo.

Wakiongea leo Jumatatu katika soko hilo, wafanyibishara, wahudumu wa matatu na waendeshaji bodaboda wameiomba serikali ya kaunti ya Kisii kukarabati na kufungua baadhi ya barabara zilioko katikati mwa mji wa Kisii ili kuzuia msomgamano huo mkubwa wa magari unaoshuhudiwa kila siku ya soko.

Kwa mujibu wa wahudumu hao, kuna baadhi ya barabara ambazo zinastahili kufanyiwa ukarabati na kufunguliwa ili ziweze kuwasaidia kwani kwa sasa wanakubaliwa kutumia barabara moja tu kuingia na kutoka katika steji, jambo ambalo husababisha msongamano mkubwa.

Wafanyibiashra waliwaunga mkono wahudumu hao na kuongeza kuwa barabara hizo zikikarabatiwa biashara itanawiri kwani masaa ya wafanyibiashara wanachukua barabarani kwa sababu ya msongamano yatapungua.

“Tunaomba serikali ya kaunti yetu kufungua baadhi ya barabara ambazo tutaweza kutumia kwani kuna barabara nyingi katika mji huu ambazo zinastahili kukarabatiwa na kufunguliwa," alihoji Kevin Mokaya, muhudumu wa matatu.

Aidha, waliomba kuwa wakati barabara hizo zikikarabatiwa, kaunti hiyo ituelezwa jinsi zitakavyotumika kama miji zingine kwani kuna mpangilio na ratiba ya barabara ya kuelekeza watu wanakoendasehemu mbali mbali, kinyume na mji wa Kisii.

“Nafahamu vyema kuwa kaunti yetu ya Kisii inaendelea kuimarika kiuchumi kufuatia ongezeko la magari na bodaboda na kwa sababu ya hayo mabadiliko, tunaomba barabara zipanuliwa kupunguza msongamano huu ambao unakera mno," alihoji Leyton Mogendi, mhudumu wa bodaboda.

Wahudumu hao waliongezea kuwa wanaimani kuwa serikali ya kaunti hiyo itawasaidia kwani sekta ya uchukuzi mjini Kisii ndio imeinua viwango vya uchumi wa kaunti hiyo kwa kuwa kuna watu wengi katika sekta hiyo.