Baadhi ya wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Kisii wamesema hawatazitumia ofisi ambazo ambazo wamejengwewa na serikali ya kaunti hiyo hadi wafanyikazi 300 walipwe mishahara yao.
Wawakilishi hao wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo Henry Moracha siku ya Jumanne walisema sharti haki itendeke kwa kwa wafanyikazi hao ambao hawajalipwa kwa muda wa miezi 10. Waliapa kutozitumia ofisi hizo hadi mishahara hio ilipwe.
Spika wa bunge hilo Okerosi Ondieki alisema kuwa suala hilo halikupangiwa kuzungumziwa kwenye kikao hicho cha bunge na kusema mwakilishi Henry Morancha aliamua kulizungumzia kwa nia ya kibinafsi wala sio kujali maslahi ya wafanyikazi hao .
“Sitaruhusu suala hilo kuzungumziwa leo maana halikuwa kwa mjadal,”alisema.
Morancha alisisitiza kuwa lazima wafanyikazi hao walipwe kabla ya ofisi hizo kutumika kama njia ya kuonyesha serikali inawatendea wakazi haki.
Aliyakanusha madai madai ya spika Ondieki ambaye alisema kuwa Marancha anahitaji kujiimarisha kisiasa.
“Naomba wafanyikazi hao walipwe mara moja tuyasahau mambo hayo,” alisema.