Share news tips with us here at Hivisasa

Wahudumu wa afya katika hospitali ya ukanda eneo la Pwani wanadai kuwa kuna haja ya kubuniwa kwa kitengo maalum cha kisheria cha kukabiliana na wabakaji ili kumlinda mtoto wa kike.

Afisa wa afya katika hospitali kuu ya ukanda wa pwani Faiza Ahmed Nassir amesema kwamba asilimia 90 ya visa vya ubakaji vinatendewa wasichana wa chini ya umri wa miaka 15 na wahusika zaidi hutoka katika jamii zao.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano, Faiza alisema kwamba visa hivyo vimechipuka kutokana na kukithiri kwa utumizi wa mihadarati na ukosefu wa ajiri miongoni wa jamii, na akasema kwamba iwapo kitengo hicho kitabuniwa, basi visa vingi kwa ubakaji katika eneo la pwani na hususan kaunti ya Mombasa vitapungua kwa asilimia kubwa.

"Tumeona kwamba kuna haja ya kitengo maalum cha kukabiliana na wabakaji kubuni ili kuona kwamba mtoto wa kike  analindwa vyema dhidi ya visa vya ubakaji na wahusika kuchukulia hatua kali za kisheria na kupunga kukithiri kwa uovu huo miongoni mwa jamii," alisema Faiza.

Afisa huyo wa afya ameyataja maeneo ya Mishomoro, Kisauni na Likoni kuwa maeneo yaliyo na idadi kubwa ya visa vya ubakaji wa wasichana wadogo pamoja na akina mama, na akasema kwamba lazima hatua hiyo kukomeshwa.