Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kennedy Otieno ambaye ni mkaazi wa mtaa wa Manyatta jijini Kisumu, alifikishwa katika mahakama ya Winam jijini Kisumu mapema Jumatatu, na kushtakiwa kwa kumpiga mamake kwa ugali.

Mahakama iliambiwa kuwa mnamo tarehe nne mwezi huu, Otieno mwenye umri wa kati ya mika 22 na 24, alimpiga mamake kwa kutumia ugali, nyumbani kwao mtaani Manyatta.

Hii ni baada ya mamake, kutaka kufahamu sababu ya yeye kurejea nyumbani akiwa amechelewa.

Otieno alikiri kosa hilo mbele ya hakimu Caroline Njalali, huku ikiagizwa kuwa mshtakiwa asalie rumande.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 14 mwezi huu, ambapo itapangiwa siku ya kusikilizwa.