Mbunge wa Nakuru mjini magharibi Samuel Arama ametoa wito kwa viongozi kutoingiza siasa katika swala la elimu humu nchini.
Akizungumza Jumamosi katika shule ya msingi ya Nakuru magharibi, Arama amesema kuwa elimu ni nguzo mhimu na wale ambao wanaingiza siasa katika swala hilo wanakosea.
Amesema kuwa serikali ya Jubilee imejitolea na yafaa kudhihirika hata mashinani kwamba elimu in nguzo muhimu na ipewe kipaumbele.
"Hii mambo ya elimu tafadhali tusiingize siasa, tunafaa kupea kipaumbele kwani ni nguzo mhimu kuwa maendeleo ya taifa," akasema Arama.
Wakati huo huo amewahakikishia wakazi wa eneo bunge lake kwamba atahakikisha elimu kuwa kila mtoto.
Arama ameongeza kuwa maswala ya ufadhili wa elimu yatazingatia haki.