Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Shughuli za upakiaji na upakuaji wa makasha na bidhaa zinazoingia katika Bandari ya Mombasa zinatarajiwa kufanyika kwa wepesi zaidi kufuatia kukabidhiwa rasmi kwa behewa la pili  almaarufu 'terminal 2' lilokuwa chini ya wahandisi walioikamilisha hivi karibuni.

Katika kikao na Waandishi wa habari kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Mombasa Catherine Mturi-wairi ameeleza kuwa terminal hiyo imekabidhiwa rasmi kwa Bandari ya Mombasa hivyo basi kuwapa nguvu ya kudhibiti shughuli za upakuaji katika sehemu hiyo

Wakati huo huo Mturi-wairi amechukua furasa hiyo pia kuweka wazi utendakazi wa Bandari ya (Kenya Ports Authority) KPA ya mwaka wa 2015 ambapo usafirishaji wa bidhaa katika mataifa yanayotumia bandari ya KPA maarufu kama 'transit' umefanya vyema huku Uganda ikiongoza kwengineko shughuli za kusafirisha bidhaa kupitia meli ikionekana kutofanya vyema.

Hata hivyo Catherine ameeleza changamoto kubwa inayo kabili KPA ni kukawia kwa makasha kupakuliwa ambapo imeonekana kuzidi kutoka siku tatu hadi siku tano.