Barabara ndio nguzo kubwa ya uchumi nchini, lakini kwa wakaazi wa Bochura eneo bunge la Kitutu Chache Kusini katika kaunti ya Kisii, barabara imekuwa kizuizi katika kukuza uchumi wao.
Ni kilio kwa wanamatatu na wanabodada wanaotumia barabara ya Nyambera-Bochura-Nyamataro.
Kulingana na wanabodaboda hao wanasema kuwa barabara hiyo ndio wanayoitumia kupata riziki yao ya kila siku, lakini sasa hawana la kutegemea haswa wakati kama huu mvua inapoanza kunya.
Wakizungumza na nasi, wameomba serikali ya kaunti ya Kisii kuingilia kati ili kuwasaidia kupata riziki.
“Hii barabara iliwekwa lami lakini ni ile mbaya hata imetoka tena yote, wakaleta 'marrum' wakati wa elinino wakamwaga mawe makubwa hata hawakutandaza vyema," alisema mwanabodaboda.
"Kuna mashimo makubwa hata unaweza ukapanda ndizi, maji na matope yamejaa katika barabara hata huwezi pita na ‘customer’ sababu anaogopa tope litamchafua," alieleza mwanabodaboda.
Tunaomba serikali itusaidie ili na sisi pia tupate riziki. Barabara hii inatumiwa na watu wengi lakini imesaulika,” aliongeza mwanabodaboda.