Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bunge la Kaunti ya Mombasa limeagiza kamati za Leba, Afya, Mazingira na ile ya Haki, kuyachunguza madai kuwa wafanyakazi wa kampuni ya kushona nguo ya EPZ, iliyooko Changamwe, waliachishwa kazi bila notisi.

Hii ni baada ya wafanyakazi hao kuandamana siku ya Jumanne hadi majengo ya bunge hilo, kuwasilisha lalama zao kwa kile walikitaja kama kudhulumiwa na wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Akizungumza siku ya siku ya Jumatano, Naibu Spika Mswabah Rashid aliagiza kuchunguza kwa swala hilo na kuwasilishwa kwa ripoti siku ya Alhamisi wiki hii.

Ililazimu bunge la kaunti kusitisha shughuli zake siku ya Jumanne kujadili swala hilo, baada ya notisi kuwasilishwa na mwakilishi mteule Mohamed Hatimy.

Inadaiwa zaidi ya wafanyikazi 2,000 wa kampuni ya EPZ waliachiswa kazi bila kupewa ilani baada ya kuchipuka madai kuwa walikuwa wanapanga kujiandikisha na vyama vya kutetea haki za wafanyikazi.

Hata hivyo, usimamizi wa kampuni hiyo bado haujatoa taarifa zozote kuyahusu malalamishi ya wafanyikazi hao.