Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Huenda mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC, Issack Hassan, akokosa kusimamia uchaguzi mkuu ujao wa 2017, endapo kura za uchaguzi mdogo wa Malindi na Kericho zitaibiwa.

Kauli hii ilitolewa na kiongozo wa wengi katika bunge la kitaifa Adan Duale siku ya Jumatatu huko Malindi.

Akihutubia halaiki katika uwanja wa Alaskani mjini Malindi, akiwa ameandamana na viongozi kadhaa wa Jubilee, Duale aliutaja uchaguzi wa Malindi na Kericho, kama kigezo cha iwapo tume hiyo inaweza kuendesha uchaguzi wa huru, haki na wazi.

Aidha, ameitaka tume hiyo kujizatiti ili kuzuia visa vya kuibiwa kura Malindi.

Duale ameitaka tume ya IEBC kuhakikisha uchaguzi mdogo wa Malindi ni wa uwazi na wa haki.

Alisisitiza haja ya kuweko kwa kura zenye uwazi, haki na zenye amani, ili kupatikane viongozi bora kwa wananchi.

Duale aliwataka wapiga kura kujitokeza kwa wingi na kuwachagua viongozi wanaowapenda.

Aidha, alisisitiza kuwa Jubilee imejitenga na siasa za matusi na chuki kwa jamii.

Haya yanajiri baada ya kushuhudiwa joto la kisiasa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Malindi.