Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua ametoa wito kwa wahudumu wa magari ya umma kuwa waangalifu barabarani.

Kinuthia alikuwa akizungumza Jumatatu eneo la Gatamaiyu, Naivasha wakati wa mazishi ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Mirera John Nganga na mwanawe George Washingtone walioaga kutokana na ajali ya barabara.

 Kinuthia alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuendelea kuwapoteza wananchi kupitia ajali za barabarani.

"Hata tunapoomboleza vifo vya wenzetu, ningependa kuwarai madereva tafadhali tuwe waangalifu barabarani,"Mbugua alisema.

Hafla hio ya mazishi ilihudhuriwa pia na naibu gavana Joseph Ruto.