Share news tips with us here at Hivisasa

Waziri wa uchukuzi James Macharia amemteua Bakari Hamisi Gowa kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la Kenya Ferry.

Gowa ambaye alihudumu kama meneja wa fedha, anachukua nafasi ya Musa Hassan aliyelazimishwa kustaafu siku ya Jumatano kutokana na huduma zisizoridhisha kaitika shirika hilo.

Kwenye barua iliyotiwa sahihi na mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo Mshenga Ruga, bodi hiyo ilipendekeza kuachishwa kazi kwa Musa ili kutoa nafasi kwa uchunguzi kubaini chanzo cha masaibu ya shirika hilo.

Waziri Macharia alitekeleza mapendekezo yaliyotolewa na bodi inayosimamia Shirika hilo.

Mhandisi mkuu Amos Nyadero ambaye alihudumu kama mhandisi mkuu pia aliachishwa kazi.

Hatua hii inajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta kuzuru makao makuu ya ofisi hizo zilizopo eneo la Likoni.