Kufuatia malumbano ya mara kwa mara na hatua ya baadhi ya viongozi kuanzisha vyama vyao kama gavana wa Bomet Isaac Ruto, mwanasiasa mmoja amepongeza hatua hiyo na kusema kuwa kila kiongozi na Mkenya yeyote anayo haki ya msingi kufuata kile anaamini kinamfaa.
Akizungumza na mtayarishi wa makala haya siku ya Jumanne eneo la Tononoka jijini Mombasa, mwanasiasa huyo, Suleiman Mwambi, alisema kuwa Isaac Ruto amechukua hatua muhimu ambayo inapaswa kufuatwa na viongozi wengine badala ya baadhi ya viongozi wengine kushinda kuwafuata wanasiasa wakongwe nchi kwa kutegemea kupewa kitu kidogo na kuwapotosha watu waliompigia kura hali ambayo alisema imekuwa mazoea kwa wengi wa viongozi wengi nchini.
Kuundwa kwa chama cha hivi karibuni na vyama mbalimbali vya Jubilee, alisema imekuwa kifungua macho kwa wanasiasa wengi wanaochipuka sasa na wana nia ya kuwania viti vya uongozi nchini.
“Nampongeza gavana huyo wa Bomet kwani ni wachache wanachukua hatua kama hiyo kwa kuhofia kukataliwa na jamii yao na wanasiasa wakuu kutoka maeneo wanatoka, hivyo kila mtu laziama apewe nafasi ya kufikiria na kufanya uamuzi nafsi bila kufuata mawazo ya wengi,” alisema mwanasiasa huyo.
Hatua hiyo ya Ruto inaoneka na wengi wa wachanuzi wa masuala ya siasa kuwa inayoshinikizwa na siasa za upinza na huenda gavana huyo akatangaza nia ya kusimama urais mwaka wa 2017.