Mmea wa miraa unafahamika kwa majina si haba kama vile alele, kiza, mairungi na kadhalika.
Mmea huu ambao una umaarufu kwa Wapwani wengi na wabara sawia kwa kile wanachokitaja kama 'starehe safi, huenda ukasababisha athari kubwa za kiafya.
Je, wajua athari za kutafuna miraa?
1. Mlaji hupata raha ya muda tu pale anapotafuna miraa na kurudia hali yake ya kawaida pindi 'steam' inapokatika.
2. Majimaji yanayotoka kwenye mmea huu hukosesha mtu usingizi.
3. Miraa pia huathiri mja kisaikolojia kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi.
4. Miraa husababisha vidonda vya tumbo kwa ukosefu wa maji ya kutosha mwilini.
5. Kwa akina mama wajawazito, unapotafuna miraa, waweza kujifungua mtoto ambaye hajakamilika kimaumbile, kwa ukosefu wa madini muhimu mwilini.
Haya basi, unapokwenda kuagizia "dharba" yako, haya nayo uyajue fika.