Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kivumbi cha kuwania wadhifa wa ugavana, Nairobi kitakuwa baina ya gavana wa sasa, Evans Kidero na Seneta Sonko.

Utafiti uliofanywa na shirika la utafiti la TIFA unaonyesha kuwa Kidero na Sonko wana wafuasi asilimia 28% ya wapiga kura katika kaunti hiyo. Utafiti huo ulifanywa kati ya Januari 31 na Februari 3 mwaka huu na ulibaini kuwa Ann Waiguru anaungwa mkono na asilimia 7% ya wapiga kura akifuatiwa na Margaret Wanjiru aliye na asilimia 4%. Johnstone Sakaja na Dennis Waweru wana asilimia 1% kila mmoja.

‘‘Utafiti huu ulifanywa baada ya fununu kuwa Ann Waiguru na Johnstone Sakaja watawania kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi. Baada ya wawili hao kutangaza kuwa watawania kiti hicho, wakenya watakuwa makini kuamua ni nani atakabidhiwa uongozi huo,’’ alisema Maggie Ireri, mkurugenzi mkuu wa shirika la TIFA.

Hata hivyo, Bi Ireri alisema asilimia 24% ya wapiga kura, Nairobi hawajafanya uamuzi kuhusu ni nani haswaa watamchagua kuwania nafasi hiyo ya ugavana katika kaunti hio.

Utafiti huu umetolewa siku chache baada ya Tume ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC kuanzisha zoezi la kuwasajili wapiga kura.