Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Naibu Kinara wa chama cha ODM Hassan Joho ameipongeza Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC kwa kuendesha uchaguzi wa huru na haki.

Joho alisema kuwa hatua ya maafisa wa IEBC kutoegemea upande wowote ndio unastahili kutekelezwa siku zote.

Akizungumza na wanahabari baada ya kutangzwa kwa matokeo ya uchaguzi huo, Joho alipongeza hatua ya wakaazi kujitokeza kwa wingi na kuungana kwa pamoja na kumchagua Willy Mtengo kuwa mbunge wa eneo hilo.

Alisema kuwa wakaazi wa eneo hilo walitekeleza jukumu lao kkwa kumteuwa kiongozi bora.

Joho alisema kuwa Mtengo anafaa kuwahudumia wakaazi wa Malindi na kuwa kiongozi mwajibikaji, ili swala la uongozi na maendeleo yatekelezwe.

“Tunawashukuru maafisa wa IEBC kwa kujitahidi kuendesha uchaguzi wa amani, huru na haki. Pia tunawashukuru wakaazi wa Malindi kwa kuonyesha ungwana na kushirikiana kumteua kiongozi shupavu Willy Mtengo. Tunawahakikishia wakaazi kuwa maswala ya maendeleo yatatekelezwa vyema Malindi,” alisema Joho.

Kwa sasa kinachosubiriwa ni kuapishwa kwa Willy Mtengo kuwa mbunge wa Malindi na kuanza shughuli za kuwahudumia Wakaazi wa Malindi katika maswala mbalimbali ikiwemo ya kimaendeleo.