Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi wa kaunti ya Kisii wameshauriwa kuwa waangalifu sherehe za krismasi na mwaka mpya zinapowadia haswa katika sekta ya usalama.

Ushauri huo umetolewa baada ya kugundulika kuwa wengi wa wakaazi si waangalifu huku wakitegemea ulinzi wa maafisa wa polisi kila wakati.

Akizungumza mjini Kisii siku ya Jumanne, kamishena wa kaunti ya Kisii Chege Mwangi aliomba wakaazi kuwa waangalifu kila wakati msimu huu wa sherehe.

Mwangi aliomba wakaazi wote wa kaunti hiyo kushirikiana na maafisa wa polisi kuhakikisha usalama ili kila mtu kuwa katika hali nzuri ya usalama.

“Naomba kila mkaazi awe mwangalifu wakati huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya. Mambo ya usalama huanza na mwananchi binasfi kwa hivyo naomba muwe macho na kushirikiana na polisi kuhakikisha usalama uko shwari katika kaunti yetu,” alisema Mwangi.

Wakati huo huo, Mwangi aliomba waendeshaji bodaboda kuwa na nidhamu wanapoendelea na shughuli zao za uchukuzi kila wakati.

Aidha, aliwataka wanabodaboda hao kuwa maakini katika uchukuzi kwa kuwasafirisha wateja wao kwa njia iliyo shwari na sio kuendesha pikipiki kwa kasi.

“Waendeshaji pikipiki naomba muwe na nidhamu barabarani mnapowasafirisha wateja wenu na muwe waangalifu na madereva wa magari pia mnafaa mfuate mtindo huo huo,” aliongeza Mwangi.