Share news tips with us here at Hivisasa

Dhehebu la PCEA limewashauri wanasiasa humu nchini kutoangazia sana siasa za 2017 na badala yake waunganisha wakenya. Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la PCEA Dr Arthur mjini Nakuru, Kasisi J Mburu alisema kuwa shida zinazoshudiwa humu nchini ni kutokana na hatua ya viongozi kuweka mawazo yao kwenye siasa za 2017.

"Viongozi wanafikiria namna watashinda uchaguzi mkuu ujao,"alisema Kasisi Mburu.

Kiongozi huyo wa kidini alirejelea matamshi ya kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis kwamba Kenya imebarikiwa lakini ingali na shida katika sekta ya elimu, afya, mazingira na familia.

"Haya mambo yalizungumziwa na papa Francis alipozuru humu nchini lakini hakuna anayetilia maanani," Kasisi Mburu alisema.