Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya kaunti ya Nyamira imeombwa kuhakikisha pesa za wanachama wa polisi jamii zimetumwa kwa kila wadi ili kutoa usaidizi kwa wanachama hao ili kuendesha shughuli zao bila shida.

Hii ni baada ya serikali ya kaunti hiyo kutenga shillingi millioni 7 kutoa huduma ya kusaidia wanachama wa polisi jamii kuleta usalama katika vijiji vya kaunti hiyo.

Akizungumza siku ya Alhamisi mjini Nyamira, mwakilishi wa wadi ya Nyansiongo Jackson Mogusu alisema kufikia sasa pesa hizo zingekuwa zimefika kwa kila wadi ili kutumika kununua bidhaa ambavyo wanachama hao hutumia katika shughli zao za kila siku.

Aidha, alisema polisi hao hupitia changamoto nyingi wanapoleta usalama na kusema kuna haja ya kusaidiwa.

Mogusu alisema sehemu za Borabu wakazi wengi hawalali kwa ukosefu wa usalama, huku wezi wakiendelea kuwahangaisha kila wakati.

“Naomba gavana wetu kuhakikisha pesa zilizotengwa kutoa usaidizi kwa wanachama wa polisi jamii zimetumwa kwa kila wadi ili usalama uimarishwe kikamifu,” alisema Mogusu.